Thursday, November 1, 2012

UDBS YAFANYA KWELI UDSM INTERCOLLEGE COMPETITION

Timu ya wanafunzi wa Kitivo cha Biashara katika chuo kikuu cha Dar es salaam imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kushinda mechi mbili dhidi ya CONAS  [1-0] na UDSL [2-1] na kuifanya kuongoza kundi hilo kwa pointi 6 ikifatiwa na COET na UDSL wenye pointi 1 huku CONAS wakishika mkia wakiwa hawana pointi.Kupitia this official blog ya wanafunzi wa UDBS na nahodha wa timu hiyo Shaki-star alikaririwa akisema "Timu yetu tumejipanga vizuri na kuhakikisha tunacheza ki-team work na kuimarisha nidhamu ndani ya timu,Hili limewezekana kutokana na ushirikiano mkubwa tunaopata toka kwa management ya UDBS kupitia viongozi wake na patroni wa michezo Dr. Francis,Tunaombwa kuhudhuria kwa wingi kwa mashabiki wetu ambao ni wanafunzi wenzetu siku ya Jumamosi Jioni ya tarehe 03-11 pale viwanja vya mabibo hostel tutakapokua tunakipiga na COET".

No comments:

Post a Comment