Tuesday, November 5, 2013

TAARIFA KWA UMMA

WIZARA YA MIKOPO; Inapenda kuwataarifu kuwa APPEAL ya MIKOPO imeanza rasmi, kwahiyo wanafunzi wajaze fomu kwenye mtandao wa bodi waprinti fomu na kuzipeleka kwa loan officer-WIZARA YA MIKOPO(DARUSO)

Friday, October 25, 2013

A NOTE FROM ACADEMIC DEAN.............DR MASOUD

There has been a mistake in the publishing of the new prospectus so there are a number of mistakes noted which will eventually bring confusion in the ongoing course registrations especially in the course to opt for the whole academic year,therefore Dr Masoud has declared  that the prospectus shouldn't be used to make the choices for which course to opt and register instead he has provided some handouts which appears to be an extract of the modified prospectus and we have placed it at MAMA NTILIE STATIONARY have it and use it to do the registration...and note in case of any queries attend to the heads of course department to solve the queries..... 

Tuesday, October 15, 2013

ARIS ACCOMODATION STATUS

ACCOMMODATION NEWS; this is to inform u that u can now log in your aris accounts and check Ur accommodation status.....for those who are allocation its announced that you should start process on 19th on Saturday......

Friday, October 11, 2013

TO ALL LOAN BENEFICIARIES

TAARIFA KWA UMMA

Ndugu wana UDSM  napenda kukufahamisha kuwa tutaanza kusaini BOOM kuanzia tarehe 21 mwezi huu,na malipo yatafanyika tarehe 25 mwezi huu huu,zoezi hili litakuwa endelevu hadi tarehe 31/10/2013.....mfahamishe na mwenzako...from wizara ya mikopo UDSM

Friday, August 23, 2013

TAARIFA KWA UMMA KUTOKA BODI YA MIKOPO KWA WAOMBAJI NA WANUFAIKAJI WA MIKOPO HII....

Leo HESLB wametoa taarifa kwa Umma juu ya idadi ya waombaji wa mikopo kama ilivyoandikwa hapa chini:

UTANGULIZI:
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inawafahamisha waombaji wa mikopo kwa mara ya kwanza, Wanafunzi wanaondelea na masomo na Umma kwa ujumla kwamba mchakato wa maombi mikopo kwa mwaka wa masomo 2013/2014 ulizinduliwa rasmi tarehe 1 Mei, 2013. Mchakato huo unaendelea vizuri na kwamba wanafunzi wengi wameweza kujaza fomu za maombi ya mikopo kwa njia ya mtandao (OLAS).

WAOMBAJI WA MIKOPO WA MARA YA KWANZA:
Utaratibu wa kujaza fomu za maombi kwa waombaji wa mara ya kwanza, unawaelekeza waombaji hao kutoa taarifa zao za kihistoria kama vile shule za sekondari walizosoma (Kidato cha IV na Kidato cha VI), hali ya mwombaji au wazazi wake kiafya na pia taarifa za mdhamini wa mwombaji mkopo. Taarifa hizo zinaiwezesha Bodi kuchambua na kujua iwapo mwombaji husika ana sifa ya kukopesheka au la. Ikumbukwe kwamba lengo la utoaji wa mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ni kuwawezesha wanafunzi wasio na uwezo wa kulipia gharama za elimu ya juu kusaidiwa kufikia malengo yao. Kwa njia ya uchambuzi huo Bodi inaweza kubaini kiasi cha mkopo unaohitajika au kiasi ambacho mwanafunzi anapaswa kuchangia katika gharama zake za elimu ya juu.Kwa vile taarifa za ufaulu katika mitihani ya kidato cha sita hazihitajiki katika hatua hii ya Mwanzo, mwombaji wa mkopo haulizwi mahali popote katika fomu yake ya maombi kuhusu kiwango cha ufaulu. Hapo baadaye Bodi itakapohitaji kuthibitisha kiwango cha ufaulu wa mwombaji itapata taarifa hizo za ufaulu moja kwa moja kutoka Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA). Kutokana na utaratibu huu, mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita mwaka 2013 anaweza kuomba mkopo hata kabla ya matokeo ya Kidato cha Sita kitaifa kutolewa. Hii ni muhimu ili kuipa Bodi muda wa kutosha kupokea maombi ya mikopo, kuchambua na kisha kupanga mikopo kwa wanafunzi stahiki watakaokuwa wamedahiliwa kwa mwaka mpya wa masomo 2013/2014

WANAFUNZI WALIOKWISHA OMBA MIKOPO:
Hadi kufikia tarehe 30 Mei, 2013, waombaji mikopo wa mara ya kwanza waliokwishakamilisha maombi yao ni 424, Waombaji wa mara ya kwanza ambao wako kwenye hatua mbalimbali za ukamilishaji ni 5,320 na wanafunzi wanaoedelea na masomo waliokwishathibitisha kuendelea kupatiwa mikopo kwa mwaka ujao wa masomo ni 60,367, kama inavyoonekana kwenye jedwali hapa chini.

HITIMISHO:
Bodi inatoa msisitizo kwa waombaji wa mikopo kama ifuatavyo:(i) Kuzingatia taratibu zote muhimu zilizowekwa kwa ajili ya maombi ya mikopo.(ii) Kutumia huduma ya msaada kwa wateja (Help Desk) kikamilifu kila wanapopata tatizo lolote katika mchakato wa ujazaji wa fomu za maombi. Huduma hiyo inapatika kwa kupiga namba 022 550 7910; kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 2 usiku siku za jumatatu hadi ijumaa na kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa 10 alasiri siku ya jumamosi.(iii) Kuzingatia muda uliopangwa wa maombi ya mikopo ambapo siku ya mwisho ni tarehe 30 Juni, 2013.

IMETOLEWA NA:

BODI YA WAKURUGENZI

BODI YA MIKOPO YA ANAFUNZI WA ELIMU YA JUU

NB:
Budget ya Wizara ya Elimu kwa mwaka wa fedha 2013/2014 ni kutoa mikopo kwa jumla ya waombaji 98,025; yaani waombaji wapya watakao pata mikopo ni watu 35,649 na waombaji wanaoendelea na masomo ni 62,376.

EXITING OPPORTUNITIES AWAITS STUDENTS

Exciting opportunity awaits students.

Dar es salaam University Finance Association(DUFA) together with YUNA and RULEX Enterprises is organizing an event for secondary school students to be held on 24th August,2013 at the University of Dar es salaam with an aim of inspiring,motivating and educating the students. Which of you guys am I going to meet there? Lets meet and share knowledge and how we are going to help each other to improve Education in Tanzania. "Educate a child, educate the future". See you there!!!!

Venue: Theathre 2 near the main library.