Taarifa nyingine kutoka
mitandao mbalimbali ya Nigeria zinasema wanafunzi hawa wanne walimchukua
mwenzao mmoja ambae anajulikana kwa ubabe ili wamtumie kumtisha huyu
anaedaiwa atoe pesa haraka, huyu jamaa waliemuongeza akawa watano
inasemekana alikua na bastola.
Wakati wa purukushani na
mdaiwa aliionyesha hiyo bastola na wakati wananchi walipokusanyika baada
ya kupigwa kelele za wezi jamaa mwenye bastola kwa uoga aliamua
kuisalimisha ile bastola ambayo ndio wananchi walipata uthibitisho
kwamba jamaa ni wezi, wakaanza kuwapiga lakini aliesalimisha bastola
akafanikiwa kukimbia wkaabaki hawa wanne ambao ndio wameuwawa.
Taarifa zote
nilizozisoma zinasema wanafunzi hawa hawakuwa wezi na wametoka kwenye
familia zenye uwezo, hata mmoja wao miezi kadhaa iliyopita alikua nchini
Marekani kwa mapumziko, ndio huyo hapo chini kwenye picha akiwa
shopping Marekani |
No comments:
Post a Comment